Na winston kinyaha
Viongozi wa Mtibwa Sugar hadi sasa wapo njia panda kufuatia
kufungiwa kwa viwanja vyake vyote ilivyokuwa inachezea mechi za nyumbani
kunako Ligi Kuu Bara.
Ikiwa ni wiki kadhaa tangu kufungiwa Uwanja wa Manungu, Mtibwa
ilipangiwa kutumia uwanja wa Jamhuri ambao nao wiki hii umetangazwa
kufungiwa na Bodi ya Ligi.
Akizungumza ofisa habari klabu ya Mtibwa, Thobias Kifaru,
ambaye aliibuka na kusema kuwa hadi sasa wapo njia panda kuwa watatumia
uwanja gani.
"Kiukweli hatujajua maana Manungu ilifungiwa na sasa Jamhuri nayo pia imefungiwa.
"Tunachoomba sisi TFF na Bodi ya Ligi waturuhusu tutumia huu wa Manungu
sababu tunaingia kwenye gharama kubwa sana kupeleka timu Jamhuri,
inakuwa kama tunaenda ugenini.
"Tunawaomba TFF watusaidie kwa hili hata kwa kipindi hiki tukiwa tunaelekea kujenga uwanja wetu wenyewe."

0 Comments: