Friday, February 10, 2023

UKWELI KIFO CHA RAPPER AKA KUPIGWA RISASI SOUTH AFRICA


Rapa AKA wa Afrika Kusini amefariki dunia kwa kupigwa risasi muda mfupi kabla ya kutumbuiza jijini Durban.


AKA ambaye jina lake halisi ni Kiernan Forbes ameuawa kwa kufyatuliwa risasi kutoka kwenye gari akiwa amesimama nje ya mgahawa.

Polisi nchini humo wamethibitisha kuwa nyota huyo mwenye miaka 35 pamoja na mlinzi wake wameuawa.

Hajafahamika sababu ya mauaji hayo, na sasa jeshi la polisi linaendelea  na uchunguzi Taarifa zinasema licha ya AKA mauaji mengine yametokea pia katika tukio husika 

"Durban - Police sources in Durban have confirmed rapper Kiernon ‘AKA’ Forbes was shot dead in a drive-by shooting on Florida Road on Friday night.

Another person believed to be AKA’s bodyguard, was also wounded, while another unidentified person, who is understood to be a close friend of AKA, has been shot dead.
It is understood that AKA was standing outside the Wish Restaurant when he was gunned down in a drive-by shooting.
The identity of the second person shot dead is unknown at this stage, but he is understood to be a close friend of AKA.

According to social media posts, AKA was due to perform at a Durban night club, YUGO, where he was expected to perform as part of his birthday celebrations."
Source : Nehanda Radio

Baadhi ya Mitandao ya Afrika Kusini ukiwemo Mtandao wa TimesLIVE na iol imeripoti kuwa Rapper huyo AKA, amefariki kwa kupigwa risasi akiwa Jijini Durban alikokua amekwenda kikazi 

Rapa AKA alikuwa na mtu wa pili aliyepigwa risasi naye ametambuliwa kuwa ni mmoja wa marafiki zake wa karibu na meneja wa zamani, Tebello 'Tibz' Motsoane. 

Tebello alikuwa amesimama nje ya Wish Restaurant akiwa na AKA na wengine wakati watu wenye silaha waliokuwa kwenye magari mawili walipofyatua risasi na kuwaua  wote wawili na kumjeruhi mtu mwingine anayesemekana kuwa ni mlinzi wa AKA. 

Tebello alimsimamia AKA miaka mingi iliyopita kabla ya kuamua njia mpya ya kazi na kuwa mpishi na kuanzisha chapa ya nguo. 

Wawili hao na wengine walikuwa wamesafiri kwa ndege hadi Durban siku ya Ijumaa, Februari 10 kusherehekea siku ya kuzaliwa ya AKA
      Aka akiwa na rafiki yake Tebello 'Tbiz'

Pia Familia Kupitia akaunti ya Instagram ya rapa huyo, famili imethibitisha kifo cha mpendwa wao @akaworldwide 

Familia imeeleza inasubiri ripoti zao kutoka Polisi na wao wamepokea kwa masikitiko hapa za kijana wao.

Imeeleza kuwa ameacha mtoto mmoja wa kike anayeitwa KAIRO.



Watu maarufu mbalimbali wa South Africa akiwemo DJ Black Coffee, Mtangazaji TBO Touch na Rapper 2FreshLES, bila kutoa maelezo ya ziada wameonesha kuwa katika majonzi kupitia kurasa zao za Twitter usiku huu.

Night Club ya YUGO ya Durban ambayo AKA alitarajiwa kuwepo usiku huu kufanya onesho na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, imetoa taarifa ya dharura saa mbili zilizopita na kusema tukio hilo limefutwa.

Rapepr AKA amewahi kufanya kazi na Wasanii wengi Afrika Burna boy , Sakodie kutoka Nigeria pia Tanzania ambao ni Diamond Platnumz kwenye wimbo wa "make me sing" ulioachiwa mwaka 2016 na "don't bother" aliofanya na Joh Makini ulioachiwa November 2015.

1 comment: